Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya haki za binadamu yalaani matumizi ya nguvu Guinea

Tume ya haki za binadamu yalaani matumizi ya nguvu Guinea

Vikosi vya usalama nchini Guinea vimeshutumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kuvunja maandamano yaliyofanyika kwenye mji mkuu wa Conakry mapema juma hili.

Tume inayohusika na haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR inasema kuwa inaamini kuwa vikosi vya usalama vilikiuka haki za bidanamu kwa kuwafyatulia risasi waandamanji wasiokuwa na silaha, kwa kuvunja na kusaka kwenye nyumba za kibinafsi na kwa kuwapiga waandamanaji .

Msemaji wa OHCHR Rupert Colville anasema kuwa mtu mmoja aliuawa na wengine 62 kujeruhiwa akiwemo kijana wa miaka saba aliyepigwa risasi kimakosa akitoka shuleni.

(SAUTI YA RUPERT COLVILE)

Tume hiyo sasa inatoa wito kwa serikali ya mpito kuhakikisha kuwa vikosi vya usalama vinafuata sheria za kimataifa kuhusu matumizi ya nguvu na silaha.