Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya elfu 30 waathirika na kipindupindu Nigeria

Watu zaidi ya elfu 30 waathirika na kipindupindu Nigeria

Takriban watu 1,555 wameripotiwa kuaga dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu na wengine 38,173 kuambukizwa ugonjwa huo nchini Nigeria .

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa hata kama ugonjwa huo umedhibitiwa bado visa vipya vinaendelea kuripotiwa kutoka kwa maeneo ambayo tayari yameathirika hususan kaskazini mashariki mwa nchi. Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa wanawake na watoto wanachukua asilimia 80 ya walioathirika.

Kulingana na shirika la afya duniani WHO ni kuwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Nigeria unasababishwa na masuala ya nyakati, mazingira machafu, na watu kusafiri kutoka eneo moja hadi lingine. Kwa sasa serikali za maeneo yaliyoathirika zinatafuta njia za kukabiliana na ugonjwa huo. Marixie Mercado kutoka UNICEF anaeleza.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)