Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza hatua ya kutoa matokeo ya awali Afghanistan

UM wapongeza hatua ya kutoa matokeo ya awali Afghanistan

Umoja wa Mataifa umekaribisha hatua ya utoaji wa matokeo ya awali katika uchaguzi wa Bunge uliofanyika mwezi uliopita nchini Afghanistan, lakini hata hivyo umeonya kuwa uchaguzi bado haujaisha.

Uchaguzi huo ambao uliratibiwa na Tume ya taifa ya uchaguzi uliwavutia wapiga kura zaidi ya milioni 4 waliojitokeza kuchagua wawakilishi kwenye bunge dogo linalojulikana kama Wolesi Jirga.Jumla ya wagombea 2,500 ikiwemo wanawake 400 wanawania viti 249 bungeni.

Akizungumzia uchaguzi huo, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Staffan de Mistura,amesifu hatua ya tume ya uchaguzi kuanza kutoa matokeo ya awali. Lakini pia amepongeza namna tume hiyo ilivyoimarisha utendaji kazi akisema kuwa hiyo ni ishara njema kwenye safari ya uimarishaji demokrasia.