Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polisi wasio na ujuzi wanatia hofu Timor-Leste :UM

Polisi wasio na ujuzi wanatia hofu Timor-Leste :UM

Idadi kubwa ya maafisa wa polisi wasio na ujuzi Timor-Leste, wanatia hofu amesema afisa wa Umoja wa Mataifa nchini humo Ameerah Haq.

Akiwasilisha taarifa kuhusu nchi hiyo kwenye baraza la usalama hii leo amesema jeshi la polisi la Timor -Leste lilishindwa kutimiza wajibu wake wakati wa machafuko ya 2006 yaliyosababishwa na maafisa wa jeshi kupinga serikali na kuufanya Umoja wa Mataifa kuchukua jukumu la polisi wa nchi hiyo.

Bi Haq amesema maafisa wa jeshi la polisi la nchi hiyo PNTL wameanza tena majukumu yao katika wilaya nyingi huku mji mkuu Dili ukisalia kuwa wenye changamoto kubwa. Amesema moja ya masuala yanayoinukia kutia hofu ni kwamba idadi ya polisi wasio na ujuzi ni kubwa tangu 2002 na wengi wamehamishiwa katika wilaya ya Dili. Ameongeza kuwa wameitaka serikali kushughulikia suala hilo na kuwathibitisha polisi hao.