Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio dhidi ya wafanyakazi wa UM Iraq

Ban alaani shambulio dhidi ya wafanyakazi wa UM Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la leo dhidi ya msafara wa uliokuwa umewabena wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa mjini Najaf Iraq.

Waliokuwa katika msafara huo ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Iraq Ad Melkert, naibu mwakilishi Bwana Jerzy Skuratowicz na wafanyakazi wa mpango wa Umoja wa mataifa Iraq UNAMI.

Wafanyakazi wote wamenusurika bila marejaha yoyote lakini mmoja wa wafanyakazi wa jeshi la usalama la Iraq ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya aliyeuawa na amewatakia nafuu ya haraka waliojeruhiwa. Ban pia amewashuruku mwakilishi wake na wafanyakazi wa UNAMI ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu ili kufanikisha mpango wa Umoja wa Mataifa na jukumu lake Iraq.

Ameongeza kuwa shambulio hili halitouzuia Umoja wa Mataifa kuendelea na juhudi zake za msaada kwa watu wa Iraq wakati huu wakijitahidi kuelekea maridhiano ya kitaifa na amani ya kudumu.