Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake ni hazina, na ukombizo wao ni wa dunia nzima:Migiro

Wanawake ni hazina, na ukombizo wao ni wa dunia nzima:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro amesema wanawake ni hazina na bila kumkomboa mwanamke basi maendeleo yatakuwa ndoto.

Akiwa mjini Nairobi katika uzinduzi wa muongo wa wanawake barani Afrika Asha Rose amesema Umoja wa Mataifa uko msitari wa mbele kusaidia ukombozi wa mwanamke barani Afrika.Akizungumza na mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Irene Mwakesi amesisitiza haja ya viongozi wa Afrika kutoa fursa zaidi ya kuwawezesha wanawake kwani wanaweza.

Binafsi amesema kama mama, mke na mwenye wadhifa wa ngazi ya juu duniani anajituma na anaamini kila mwanamke anaweza kuwa kama yeye hata zaidi ya yeye. Msikilize akinena na Irene.