Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi zaidi kupelekwa Sudan wakati wa kura ya maoni:UM

Vikosi zaidi kupelekwa Sudan wakati wa kura ya maoni:UM

Umoja wa Mataifa umeahidi kuongeza nguvu zaidi nchini Sudan ili kudhibiti hali yoyote inayoweza kuvuruga na kuchafua zoezi la upigaji kura ya maoni ulipangwa kufanyika Janury 9 mwakani.

Eneo la Sudan Kusin linatazamiwa kupiga kura hiyo kama ijitenge toka sehemu ya Sudan na kujiundia dola yake yenyewe. Hatua hiyo inafuatia makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2005 ambayo yalimaliza mapigano ya miongo kadhaa.

Kiongozi wa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan, UNMIS, Haile Menkerios, amesema kuwa umoja wa Mataifa uko tayari kupeleka wanajeshi wa akiba wa kulinda amani ili kuendeleza juhudi za kupiga doria. Hata hivyo amesisitiza kuwa hatua ya kutumwa vikosi ziadi katika eneo hilo, lazima kwanza iamuliwe na baraza la usalama.

Kiongozi huyo amesema kuwa wakati huu ambao wa kuelekea kwenye tarehe ya upigaji kura, ni wakati muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote hivyo lazima tahadhari ya mapema ichukuliwe sasa.