Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Iraq wasita kurejea nyumbani

Wakimbizi wa Iraq wasita kurejea nyumbani

Utafiti uliofanywa miongoni mwa Wairaq wanaorejea nyumbani kutoka nchi jirani umebaini kwamba wengi wao hawafurahii kurejea nyumbani wa wako tayari kuomba hifadhi upya.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR waliorejea wanakabiliwa na hali mbaya ya uchumi, usalama mdogo na ukosefu wa huduma muhimu jambo ambalo limewafanya kujutia aumuzi wao wa kurudi nyumbani. Melissa Fleming msemaji wa UNHCR anasema moja ya changamoto kubwa ya Wairaq wanaorejea ni kupata ajira.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Iraq wakimbizi 18,240 wamerejea nyumbani kati ya Januari na Agost mwaka huu. UNHCR inasema haichagizi watu hao kurejea Iraq ingawa inaendelea kuwasaidia wanaotaka kurejea nyumbani kwa hiyari.