Muda ndio kiini cha kuendelea kwa mazunguimzo ya mashariki ya kati

18 Oktoba 2010

Naibu mkuu wa wa idara ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kisiasa amesema kuwa hatua za haraka zinahitajika kwenye mazungumzo ya kuafuta amani kati ya Israel na Palestina.

Akilihutibia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Oscar Fernandes -Taranco amesema kiuwa majuma sita baada ya kuanza kwa mazungumzo ya moja kwa moja katika ya Isreal na Palestina mjini Washington D.C.mazungumzo hayo yamevunjika na pande zote mbili hazijakutana tangu tarehe 15 mwezi Septemba.

(SAUTI TARANCO)

muda ndio kiini na tuhataji maendeleo kwa majuma yajayo.Katibu mkuu anaendelea kuamini kuwa ikiwa lango kwenda kwa litafungwa ityakluwa vigumu kulifungua tena, Hakuna njia nyingine ya kuafikia makubaliano itakayopelekea kuundwa kwa taifa huru la Paletina wanaoshi kando na taifa la Israel kwa mani na usalama

Bwana Fernandez-Taranco ameongoza kuwa ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi kwenye ukingo wa magharibi umenza tena na rais wa palestina Mahmoud Abbas amesema kuwa hatarejea kwenye mazungumzo hayo iwapo Israel haitasitisha ujenzi huo

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter