Manufaa ya gesi ya Carbon kwa jamii

18 Oktoba 2010

Shughuli za Kutambua maeneo ya nchi yaliyo na gesio nyingi ya Carbon husan maeneo kunako patikana idadi kubwa ya wanyama wa porini na muhimu kwa wenyeji, zimeanzishwa barani Asia , Afrika na Amerika ya Kusini.

Lengo kuu ni kusaidia juhudi za kimataifa za kulinda misitu ili kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa. Njia hizi pia zina manufaa mengine kama vile kulinda maji na udongo wenye rutuba . Chini ya makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa serikali zinajadiliana mbinu za kupunguza hewa inayochafua mazingira hususan kutokana na uharibifu wa misitu lengo likiwa kupunguza uharibifu wa misitu kwa nusu ifikapo mwaka 2020. Mkurugenzi wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Achim Steiner amesema kuwa lengo ni kuwekeza katika gesi ya Carbon. Amesema kuwa Shughuli hiyo inaonyesha kuwa karibu robo ya gesi ya Carbon iliyo Tanzania inapatikana katika maeneo ambayo hayajalindwa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter