Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umasikini na njaa ni changamoto kubwa nchini Kenya

Umasikini na njaa ni changamoto kubwa nchini Kenya

Umasikini na njaa ni changamoto kubwa nchini kenya kama ilivyo kwa mataifa mengi ya Afrika.

Na hilo ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na ni lengo namba moja la milenia ambalo linahitajika kufikiwa hapo 2015. Hadi hii leo asilimia kubwa ya raia wa nchi hiyo wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku. Huduma muhimu kama malazi, chakula na malazi bado ni dhiki na wengi wakishindwa kumudu hata milo miwili kwa siku.

Serikali ya Kenya inasema imejitahidi na ina imani kubwa kwamba ikiwa imesalia miaka mitano tuu kabla ya muda wa mwisho kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia kufika hapo 2015, itaweza kuyafikia. Mwandishi wetu kutoka Nairobi Jason Nyakundi amefuatilia na kutathimini hali halisi na ametayrisha makala hii. Ungana naye.