UM wakaribisha uteuzi wa waziri mkuu mpya Somalia
Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Augustine P. Mahiga amepongeza uteuzi wa waziri mkuu mpya wa Somalia Mohamed A. Mohamed.
Uteuzi huo ulifanywa jana na rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed. Mahiga amesema jumuiya ya kimataifa inatarajia kwamba serikali mpya ya Somalia itateuliwa hivi karibuni ili kujikita katika majukumu ambayo ni muhimu ili kufanikisha kipindi cha serikali ya mpito kitakachomalizika Agosti 2011.
Ameongeza kuwa muda hautoruhusu machafuko zaidi ndani ya uongozi wa Somalia, na kwamba Umoja wa Mataifa na mashirika wa kimataifa wako tayari kuisaidia serikali mpya chini ya uongozi wa Mohamed A Mohamed.
Serikali ambayo haijakuwa na serikali imara tangu 1991 , pia kusam,baratishwa na miongo ya vita na mgawanyiko wa kikoo, na hivi karibuni wanamgambo wa Kiislam wa al-Shabaab , inakabiliwa pia na matatizo makubwa huku watu milioni 3.2 ikiwa ni asilimia 40 ya watu wote wanahitaji msaada.