FAO yawateua mabalozi wema wanne wapya
Wasanii wanne mashuhuri wameteuliwa kama mabalozi wema wa shirika la mazao na chakula la Umoja wa Mataifa FAO kusaidia katika kampeni ya dunia ya kukabiliana na njaa.
Mkurugenzi wa shirika la FAO Jacques Diouf amewateua mcheza filamu raia wa Italia Raoul Bova, mwanamuziki kutoka Canada Celine Dion, mwanamuziki raia wa Ufilipino Lea Salonga pamoja na mcheza filamu raia wa Marekani Susan Sarandon wakati wa kuadhimishwa kwa siku ya chakula duniani mjini Rome kwenye sherehe zilizohudhuriwa pia na rais wa Rwanda Paul Kagame