Leo ni siku ya kimataifa ya kunawa mikono kwa sabuni

15 Oktoba 2010

Huku leo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kuosha mikono duniani yenye kauli mbiu "zaidi ya siku"shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa kauli mbiu hiyo ina lengo la kulifanya zoezi hilo rahisi la kuokoa maisha kuwa mazoea baada ya Oktoba 15.

Kulingana na UNICEF watoto wa shule, walimu,wazazi watu mashuhuru na maafisa wa serikali zaidi ya milioni 200 wanatarajiwa kuosha mikono kwa sabuni kuadhimisha siku hii. UNICEF inasema kuwa uoshaji wa mikono utafanyika kwa zaidi ya nchin 80 kutoa hamasisho mashuleni na kwa jamii juu ya manufaa ya kuosha mikono kwa kutumia maji na sabuni.Nchini Pakistan shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuawa linasambaza vifaa vya usafi na habari kuhusu afya kwa waathiriwa 10,000 wa mafuriko. Maelfu ya familia zinazoishi katika mazingira chafu wanapata hamasisho kutoka IOM kuhusu usafi na jinsi ya kuzuia kuambukizwa maradhi katika siku hii. Madaktari 12 na wauguzi 16 wanawahamasisha waathiriwa 10,000 wa mafuriko katika maeneo ya Punjab na Sindh kuhusu usafi , kuchemsha maji , kuosha mikono na kulinda usafi

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter