Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima mfumo wa uendelezaji kilimo duniani ubadilike:De Schutter

Lazima mfumo wa uendelezaji kilimo duniani ubadilike:De Schutter

Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki ya kupata chakula amesema kuwa lazima dunia ifike pahala kutambua kuwa inawajibika kulinda vizazi vya baadaye kwa kutilia mkazo kilimo ambacho hakileti mathara kwa mazingira.

Olivier De Schutter ambaye kauli yake ameitoa wakati kamati ya kimataifa juu ya usalama wa chakula inakutana huko Rome ameeleza kuwa, dunia bado haijawa salama kuondokana na baa la njaa. Amesema licha ya watu zaidi ya bilioni 1 kukubwa na njaa duniani kote, hata hivyo hakuna ishara njema kwani mwonekano mpya wa uendelezaji kilimo unazalisha kitisho kingine ambacho huenda kikashuhudia familia zijazo zikiwa kwenye wakati mguu zaidi.

Kwa maana hiyo ametaka kuzingatiwa kwa agenda mpya ya uendelezaji kilimo kisichotoa carbon nyingi na kuongezwa msukumo kwenye utumiaji wa pembejezo za kisasa na endelevu