Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID na viongozi wa Darfur wajadili matatizo ya wakimbizi wa ndani

UNAMID na viongozi wa Darfur wajadili matatizo ya wakimbizi wa ndani

Maafisa wa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, wamekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa eneo hilo wanahusika na makambi yanayohudumia wakimbizi wa ndani.

Katika miezi ya hivi karibuni kuliibuka machafuko ya umwagaji wa damu katika kambi ya Kalma yakiwahusisha wale wanayoyaunga mkono majadiliano ya Doha, Qatar dhidi ya wale wanayoyapinga. Kabla ya kuibuka upya wa machafuko hayo,kambi hiyo ilikuwa ikihifadhi wakimbikzi 82,0000.

Walipokutana na Naibu Mwakilishi wa vikosi hivyo vya kulinda amani UNAMID, Margaret Carey,viongozi wa eneo hilo walielezea mahitajio yao muhimu ambayo ni pamoja na kukosekana kwa hali ya usalama, chakula, elimu na upatikanaji wa elimu kwenye kambi hiyo ya wakimbizi. Bi Carey ameeleza matumaini ya kutatuliwa kwa changamoto hizo katika hali ya amani.