Hatua mpya zatangazwa na UM kusaidia masuala ya amani

14 Oktoba 2010

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza hatua zitakazochukuliwa kuimarisha jukumu la UM la kusaidia nchi zilizokumbwa na mizozo kupata amani hususan kupitia kutumwa kwa haraka kwa wafanyikazi waliopata mafunzo, ufadhili wa kifedha,ushirikiano na kuhakikisha kuwa wanawake wameshirikishwa.

Akilielezea baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu juhudi za UM katika kuleta amani kwenye nchi zilizokumbwa na mizozo Ban amesema kuwa kupatikana kwa amani kunahitaji uvumilivu, kujitolea kwa muda mrefu na kuwashirika watu wengi wanaoshirikiana. Ban anasema kuwa wamepigia hatu katika kuleta amani nchini Burundi, Haiti, Nepal, Sierra Leone na sehemu zingine.

Hata hivyo Ban amesema kuwa kuna umuhimu kwa wafanyikazi wa umoja wa mataifa wanaotumwa kwenye maeneo yaliyo na mizozo kupewa mafunzo yanayohitajika ili kuwawezesha kuutekeleza wajibu wao kwa njia inayohitajika.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter