Skip to main content

Simu za mkononi zinawasaidia masikini kiuchumi:UNCTAD

Simu za mkononi zinawasaidia masikini kiuchumi:UNCTAD

Simu za mkononi zimeelezwa kuchukua jukumu kubwa la kuwasaidia watu masikini kuinua kipato chao na hali ya maisha.

Kwa mujibu wa ripoti ya uchumi ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa biashara na maendeleo UNCTAD kwa mwaka huu wa 2010 kumekuwa na ongezeko kubwa la biashra ndogondogo za simu za mkononi.

Biashara hizo ni pamoja na kulipisha fedha kupiga simu, kufanya matengenezo na kusambaza taarifa muhimu kwa kutumia simu hizo. Torbjorn Fredriksson ni afisa wa UNCTAD anasema simu za mkononi zina faida nyingi.

(SAUTI YA TORBJORN FREDRIKSSON)