Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni dhidi ya sotoka kumalizika na ugonjwa kutokomea:FAO

Kampeni dhidi ya sotoka kumalizika na ugonjwa kutokomea:FAO

Juhudi za kimataifa zilizochangia kuupeleka ugonjwa wa ng\'ombe wa sotoka ukingoni zinamalizika na kutoa fursa ya kutokomezwa rasmi kwa ugonjwa huo hatari.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya binadamu kufanikiwa kumaliza kabisa ugonjwa wa mifugo na ni mara ya pili kutokomeza kabisa ugonjwa hatari baada ya ndui mwaka 1980.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO sotoka haidhuru binadamu moja kwa moja lakini inaweza kuangamiza kabisa idadi kubwa ya ng'ombe na wanyama wengine wenye kwato na kuleta athari kubwa kwa kilimo , kuleta njaa na uchumi.Dr Modibo Traore ni mkurugenzi mkuu msaidizi wa FAO .

(SAUTI YA DR MODIBO TRAORE)

Sotoka imeathiri Afrika, asia na Ulaya, imesasabisha kupotea kwa mamilioni ya mifugo na kuleta njaa . Hayo yameyasemwa kwenye kongamano la kimataifa la kutokomeza sotoka mjini Rome Italia lililojumuisha mawaziri kutoka nchi mbalimbali wanachama wa FAO , wataalamu wa afya ya mifugo na wadau wengine. Kongamano hilo la siku mbili linamalizika leo ukiwa ni maandalizi ya kuadhimisha siku ya chakula duniani Oktoba 15 ambayo kauli mbiu yake mwaka huu ni tuungane dhidi ya njaa.