Skip to main content

Marekani na Somalia lazima mridhie haki za watoto:UM

Marekani na Somalia lazima mridhie haki za watoto:UM

Mkuu wa tume ya uchunguzi ya umoja wa Mataifa leo ametoa witio wa Somalia na Marekani nchi mbili pekee ambazo hazijaridhia mkataba wa haki za mtoto kufanya hivyo mara moja.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya haki za mtoto Yanghee Lee ameliambia baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa kumlinda mtoto anarejea wito wake kwa mataifa hayo mawili kutia mkataba haraka iwezekanavyo. Jayson Nyakundi na taarifa kamili

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Mkataba huo ndio wa kwanza wa kimataifa wa kulinda haki za watoto walio chini ya miaka 18 zikiwemo haki za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Bibi Lee anasema kuwa bado nchi 30 zinaruhusu kuingizwa kwa watoto walio nchini mika 18 jeshini akisema kuwa bado nchi nyingi zina sheria inayowakandamiza watoto wanaoingia kwenye ukahaba badala ya kuwachukulia kama waathiriwa.

Lee anasema kuwa kuna hali ya kutatanisha kuwa wakati mkataba huu unapoidhinishwa wazazi wataacha majukumu yao ya kuwalea watoto na watoto kuchukua haki zao kutoka kwa wazazi. Lakini hata hivyo anasema kuwa hilo si kweli kwa kuwa mkataba huo unatoa wito kwa wazazi kuwapa mwelekeo watoto wao.