Tunaungana na dunia kufurahia uokozi wa wachimba madini Chile:UM

Tunaungana na dunia kufurahia uokozi wa wachimba madini Chile:UM

Uokozi wa wachimba madini 33 wa Chile waliokwama mgodini kwa zaidi ya miezi miwili umekaribishwa na kupongezwa na Umoja wa Mataifa.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO Juan Somavia amesema akiwa kama mkurugenzi wa ILo na raia wa Chile anaungana na mamilioni ya watu kote duniani kufurahia kuokolewa kwa wachimba madini hao.

Pia amewapongeza wote walioshiriki katika juhudi, ujuzi na umakini wa kazi ya uokozi, kutoka sekta binafsi, za umma, Wachile na wasio wachile, kwa mchango wao mkubwa na mshikamano wa kunusu maisha ya watu hao 33.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa unaungana na watu wa Chile na familia za wachimba madini hao kusherehekea tukio hilo la kihistoria na mshikamano ulioonyeshwa, amesema waokozi wamefanya kazi bila kuchoka, bila kukata tama na wote tunaliita tendo hilo ni la kishujaa tunalopaswa kuiga.