Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada unahitajika kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa:ADF

Msaada unahitajika kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa:ADF

Viongozi wa Afrika lazima wapatiwe fedha na nchi tajiri ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Huo ni ujumbe uliotolewa kwenye kongamano kwa ajili ya maendeleo barazani Afrika ADF linaloendelea mjini Addis Ababa Ethiopia. Kongamano hilo limesema Afrika ambayo imechangia kidogo sana katika gesi ya viwandani ndio bara linaloathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa.

Rais wa zamani wa Botswana Festus Mogae ni miongoni mwa waandaaji wa kongamano hilo anasema ingawa Afrika imechangia kidogo lakini ni wajibu wa kila mmoja kukabiliana na hali hiyo lakini kuna haja na haki ya Afrika kusaidiwa.

(SAUTI YA FESTUS MOGAE)