Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Magonjwa yanayopuuzwa yanazidisha umasikini:WHO

Magonjwa yanayopuuzwa yanazidisha umasikini:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema adha na ulemavu unaosababishwa na aina ya magonjwa sugu ya kuambukiza husussani katika watu masikini hivi sasa zinaweza kupunguzwa.

Hayo yamo katika ripoti ya shirika hilo iliyozinduliwa leo iitwayo kufanya juhudi kukabiliana na athari za kimataifa za magonjwa yaliyopuuzwa. Ripoti hiyo inagusia magonjwa 17 ambayo hughubika maeneo masikini na yanayopuuzwa kama anavyofafanua Dr Lorenzo Savioli wa WHO

(SAUTI YA DR LORENZO SAVIOLI)

Magonjwa hayo yanaweza kusababisha upofu, makovu na ulemavu wa maisha, vitonda vya tumbo, maumivu makali, ulemavu wa viungo, matatizo ya akili, kudumaa na kuathiri viungo vya ndani ya mwili. Magonjwa hayo ni pamoja na ukoma, kichaa cha mbwa, kichocho, vikope, homa ya manjano na malale. Nchi 149 zinaguswa na tatizo hili na maisha ya watu bilioni moja yameathirika.