Mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa misaada yanaongezeka

Mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa misaada yanaongezeka

Mkuu wa ujumbe wa Muungano wa Ulaya kwenye Umoja wa Mataifa amesema mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa misaada yameongezeka sana.

Balozi Pedro Serrano akizungumza wakati wa kuwasilisha tipoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ulinzi na usalama wa wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa amesema kwa mwaka jana pekee wafanyakazi zaidi ya 100 wameuawa na takribani 90 kutekwa nyara.

Ameongeza kuwa mazingira ambayo wafanyakazi wa misaada wanafanya kazi zao hasa kwenye maeneo ya vita yamekuwa ni ya hatari zaidi. Amesema nembo na bendera ambazo awali zilikuwa kama ngao kwa wafanyakazi wa misaada sasa ndio zinalengwa.

Haya mahsmbuzli yanayochochewa kisiasa na mengineyo yanatia hofu. Idadi ya waliouawa ni mara tatu ya zaidi ya ilivyokuwa miaka 10 iliyopita na waliotekwa mwaka jana pekee ni mara nne ya miaka 10 iliyopita.