Skip to main content

UM wasisitiza umuhimu wa waangalizi kwenye uchaguzi Ivory Coast

UM wasisitiza umuhimu wa waangalizi kwenye uchaguzi Ivory Coast

Kiongozi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutuma waangalizi wa kutosha kwenye uchaguzi wa uarais wa taifa hilo la afrika magharibi unaotarajiwa kundaliwa tarehe 31 mwezi huu.

Akiongea kwenye warsha ya waangalizi wa kimataifa mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na kiongozi wa Ujumbe unaofahamika kama UNOCI  Y . Choi amesema kuwa waangalizi wengi wanaofanya kazi pamoja wanaweza kufanya kazi hiyo jinsi inavyohitajika.

Bwana Choi amesema kuwa ujumbe wa UNOCI imefanikiwa kutoa usaidizi kwa tume huru ya uchaguzi nchini Ivory Coast . Uchaguzi nchini Ivoy Coast ulitarajiwa kuandaliwa kwanza mwaka 2005 lakini umekuwa ukihairishwa ukiwemo ule uliotarajiwa kuandaliwa mwezi machi mwaka huu.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalizuka mwaka 2002 na kuigawanya nchi hiyo mara mbili kati ya eneo la kaskazini linalodhibiotiwa na waasi na la Kusini lililo chini ya Serikali.