Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utawala wa kisheria ni muhimu kufikia malengo ya amani:Migiro

Utawala wa kisheria ni muhimu kufikia malengo ya amani:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro amehimiza umuhimu wa kuzingatiwa utawala wa kisheria ili kufikia shabaya ya kuwa na amania ya dunia.

Bi Migoro amesema kwa kutilia uzito uimarishwaji wa mamlaka na kuwepo kwa utawala wa kisheria miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja kutasukuma mbele harakati za amani na hatimaye kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya kuwa na amani duniani kote.

Hata hivyo amesisitiza haja ya kuendeleza juhudi za kupunguza umaskini kwani amedai kuwa utawala wa kisheria hauwezi kuwa umekamilika pasipo kufikia shabaya ya kukabili umaskini.

Bi Migiro ambaye alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa Kamati ya Baraza la Umoja wa inayohusika na masuala ya sheria, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi kwenda kinyume na misingi ya utawala wa sheria na kujitafutia kinga ili wasifikishwe kwenye mikono ya haki pindi wanapotakiwa.