Matatizo ya maendeleo Afrika yanaweza kutatuliwa:ADF

Matatizo ya maendeleo Afrika yanaweza kutatuliwa:ADF

Kongamano la saba la maendeleo barani Afrika leo limeendelea mjini Addis Ababa Ethiopia. Mada mbalimbali zinazokuwa kikwazo cha maendeleo hayo zinajadiliwa.

Miongoni mwa mada hizo ni changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la idadi ya watu, masuala ya afya, usawa wa kijinsia, kuwawezesha wanawake, ajira na masuala ya watoto.

Mawaziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika, jumuiya za kijamii, mashirika , wataalamu wa maendeleo na wadau wengine wanahudhuria na wanasema kuna matumaini kama juhudi zikifanyika Afrika itakabili changamoto hizo.

Beatrice Lalonde ni waziri wa zamani wa mazingira na ni balozi wa sasa wa Ufaransa wa mabadiliko ya hali ya hewa mfuko wa maendeleo kwa Afrika ADF.

(SAUTI YA BRICE LALONDE)