Skip to main content

Waathirika wa kubakwa DR congo wasaidiwe:UM

Waathirika wa kubakwa DR congo wasaidiwe:UM

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaoongozwa na naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu umewasikiliza baadhi ya waathirika wa ubakaji hasa katika maeneo ya vijijini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ujumbe huo umekuwa na mazungumzo na manusura wa ukatili wa kimapenzi na wadau wengine katika miji sita iliyoko kwenye majimbo matatu tofauti unajukumu la kujadili njia muafaka iliyopo na msaada kwa waathirika wa ubakaji .

Mbali ya naibu kamishina wa haki za binadamu Kyung-wha Kang, jopo linajumuisha pia waziri wa zamani wa ulinzi wa finland Bi Elizabeth Rehn na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya mfuko wa ICC kwa waathirika na daktari wa hospitali ya Panzi Bukavu Denis Mukwege. Likiwa nchini Congo linafanya kazi kwa ushirikiano na wizara ya sheria na haki za binadamu na wizara ya jinsia, familia na watoto.

Tangu tarehe 30 Septemba hadi 10 Oktoba jopo hilo limezuru Bukavu, Shabunda Kivu ya kusini, Bunia na Komanda jimbo la oriantale na Mbandaka na Songo Mboyo jimbo la Equateur na huko wamekutana na jumla ya waathirika 61 wenye umri wa kuanzia miaka mitatu hadi 61 wakiwemo wanaume wane. Jana jopo hilo lilizungumzia mambo waliyobaini na maafisa wa serikali, jumuiya za kijamii na wawakilishi wa umoja wa Mataifa mjini Kinshasa.