Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zaidi zisaidie kuwachukulia hatua maharamia:UM

Nchi zaidi zisaidie kuwachukulia hatua maharamia:UM

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu sheria za uharamia ametoa wito kwa nchi zaidi kuisaidia Kenya kuwachukulia hatua maharamia wa Kisomali.

Bwana Jack Lang ameyasema hayo huku kukiwa na hofu ya Kenya kutumiwa kama jalala la maharamia wanaowinda meli kwa ajili ya kujipatia mamilioni ya dola kama kikombozi baada ya kuziteka.

Bwana Lang amesema hofu ya Kenya kuhusu suala hilo inaeleweka na huenda itataka kufanya makubalino mapya kwa ajili ya kuchukua washukiwa wa uharamia.

Hivi sasa nchi hiyo inawashikilia maharamia 136 kati ya wafungwa wake 53,000. Jayson Nyakundi na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Lang anasema kuwa kwa sasa Kenya inabebeba jukumu kubwa na hadi sasa inawazuiliwa magharamia takriban 136. Mwezi uliopita Kenya ilisema kuwa makubaliono na Uingereza , Marekani na Jumuiya ya Ulaya kuwafungulia mashataka washukiwa wa uharamia yamepita.

Hata hivyo Lang anasema kuwa moja ya suluhu ni kuwarejesha maharamia hao nchini Somalia ili kutumikia vifungo gerezani. Somalia haijakuwa na serikali kwa miaka 20 lakini hata hiyo sehemu za Puntland na Somaliland zilizojitangaza kuwa hurU zishawafungulia mashtaka maharamia. Kwa sasa maharamia nchini Somalia wanashikilia meli 18 na mabaharamia 400 baada ya kuiteka nyara meli ya Japan Jumapili iliyopita.