Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kifua kikuu kinaweza kutokomezwa ifikapo 2015:WHO

Kifua kikuu kinaweza kutokomezwa ifikapo 2015:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema dunia iko mbioni kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu katika miaka mitano ijayo endapo serikali na wahisani wataongeza juhudi na msaada wao katika kuzuia na kutibu ugonjwa huo.

Ikizindua mkakati mpya wa kukomesha kifua kikuu ifikapo 2015 WHO imesema inahitaji dola bilioni 37 ili kufadhili utafiti wa chanjo, vipimo vya kisasa vya uchunguzi wa ugonjwa huo na mfumo wa matibabu.

WHO inakadiria kwamba watu milioni 10 watakufa na kifua kikuu katika miaka mitano ijayo kama mpango mpya wa kimataifa hautopata fedha za kutosha. Dr Philippe Glaziou ni mtaalamu katika kitengo cha kifua kikuu cha Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA DR PHILIPPE GLAZIOU)

WHO inasema kifua kikuu ni tatizo kubwa la kiafya duniani na kila mwaka kuna kuwa na wagonjwa wapya milioni 9 na inakadiriwa milioni mbili kati yao hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa huo.