Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la UM limewachagua wajumbe wapya watano wasio wa kudumu kwenye baraza la usalama

Baraza Kuu la UM limewachagua wajumbe wapya watano wasio wa kudumu kwenye baraza la usalama

Wajumbe wapya watano wasio wa kudumu wa baraza la usalama wamechaguliwa leo na baraza kuu la Umoja wa mataifa kuhudumu katika kipindi cha miaka miwili.

Wajumbe wa sasa 15 wa baraza la usalama wana jukumu la kuhakikisha usalama na kutatua migogoro kote duniani. Katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo Colombia, Ujerumani, India na Afrika ya Kusini wamechaguliwa kama wajumbe wapya.

Na upinzani baiana ya Canada na Ureno uliingia katika duru ya pili na kisha Canada ikajiengua na kutoa fursa kwa Ureno kuwa mmoja kati ya wajumbe wapya watano. Katika baraza la usalama kuna wajumbe 10 wasio wa kudumu na kuna wajumbe 5 wa kudumu ambao hupiga kura katika maamuzi yote muhimu ambao ni Uchina, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Marekani.