Nchi za Caribbean zatakiwa kukabiliana na unyanyasaji wa wanawake

12 Oktoba 2010

Nchi zilizoko katika eneo la Caribbean zimetolewa mwito kujiunga na harakati zenye shabaya ya kumaliza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon mnano wakati eneo hilo likizindua kampeni yake inayotaka kuunganisha nguvu ili kukabiliana na vitendo hivyo. Kampeni hiyo ambayo inafahamika kama UniTe, inazitaka nchi zote kwenye eneo hilo kuchukua hatua za makusudi ikiwemo kuwepo kwa sheria imara na ukusanyaji wa takwimu za uhakika, ili kukabiliana na tatizo la unyanyasaji kwa wanawake.

Kampeni hiyo imeweka shabaya hadi ifikapo mwaka 2015 vitendo vya unyanyasaji wa kingono na kijinsia viwe vimetokomezwa kabisa. Wakati akizindua kampeni hiyo Katibu Mkuu Ban ametaka kila mmoja ahusike kwenye harakati hizo,na akataka iwahusishe wanafunzi mashuleni, wafanya biashara ndogondogo masokoni mpaka katika bunge.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter