Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wanawake unaongezeka duniani:CEDAW

Ukatili dhidi ya wanawake unaongezeka duniani:CEDAW

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za wanawake imesema licha ya hatua zilizopigwa katika kutambua haki za wanawake duniani bado kuna changamoto.

Kauli hiyo imetolewa na makamu mwenyekiti wa kamati ya kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake CEDAW alipohutubia wanachama wa Umoja wa Mataifa kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa hii leo.

Bi Xiaoqaio Zou amesema changamoto zilizosalia ni pamoja na ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na hasa ukatili wa kimapenzi ambao umesambaa katika sehemu mbalimbali duniani na unaongezeka.

Ameongeza kuwa ukioukwaji huu wa haki za wanawake mara nyingi hutokea katika jamii zinazofuata mfumo dume, ambao sheria, miala na desturi zinamkandamiza mwanamke na kumkweza mwanaume.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA wanawake wanaendelea kubakwa, kuuawa kwa misigi ya mila na dini na kukumbana na mifumo mingine ya ukatili, huku waliowatendea unyama huo wakiendelea kukwepa mkono wa sheria kote duniani.