Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji haramu Afrika Mashariki udhibitiwe:IOM

Usafirishaji haramu Afrika Mashariki udhibitiwe:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limetoa wito wa kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu katika eneo la Afrika ya Mashariki.

Kwa mujibu wa shirika hilo uchunguzi uliofanywa kuhusu usafirishaji haramu wa watu kati ya Kenya na nchi jirani umebaini jinsi suala hilo lilivyokita mizizi na kuwalenga watu wa kila rika na kila jinsia. Sasa shirika hilo linataka juhudi zinafanyike kabla hali haijawa mbaya zaidi na kushindikina akuthibitiwa. Jayson Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Kulingana na ripoti iliyotolewa kwenye warsha ya shirika la IOM nchini Kenya kuhusu usafirishaji haramu wa watu katika eneo la afrika mashariki ulionyesha kuwa hata kama huenda watu wamesafirishwa kwenda nchi zingine kwa lengo la kutafuta ajira nzuri mara nyingi huwa wamedanganywa na wengine wakiwemo watu wa familia , dini, wafanyibiashara na makahaba waliostaafu kwenda kutafuta ajira nzuri.

Nchini Kenya uchunguzi huo ulionyesha kuwa watu waliosafirishwa kiharamu kutoka Rwandan, Tanzanian na Ugandan wakiwemo watoto wanafanya kazi mjini Nairobi kama wafanyikazi wa nyumbani , kwenye biashara ya ukahaba na shambani sehemu mbali mbali za nchi. Nchini Tanzania IOM iligundua usafirishaji haramu wa watoto kutoka Burundi, Rwanda na Uganda wanaofanya ukahaba , uvuvi , kazi za nyumbani na shambani.