Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka nchi za Kiarabu kusaidia Palestina kwa hali na mali

Ban ataka nchi za Kiarabu kusaidia Palestina kwa hali na mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa nchi za Kiarabu wanaokutana huko Sirte Libya kutoa uugwaji mkono wa dhati kwa kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas ambaye amedai kuwa yupo kwenye kipindi kigumu.

Wito huo ameutoa mnamo wakati mazungumzo ya ana kwa ana baina ya Palestina na Israel yakiwa katika hati hati ya kuvunjika, kufuatia kuanza ujenzi wa makazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi

Katika ujumbe huo uliotolewa kwa niaba yake na Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa wa amani ya Mashariki ya Kati Robert Serry, Bwana Ban amemuelezea Kiongozi wa Palestina kama mtu mwenye nia dhabiti ya kuona kwamba taifa lake linapata haki zake na amedhihirisha namna alivyotayari kufikia makubaliano ya usakaji amani.

Amewahimiza viongozi wa nchi za kiarabu kuongeza uugwaji mkono kusaidia ujenzi mpya wa kiuchumi na kisiasa kwa Palestina. Ameonya kuwa iwapo mazungumzo hayo ya usakaji amani yatavunjika itawia vigumu kuyafufua upya.

End