Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM waitaka China kuheshimu haki za binadamu na kuwaachilia wafungwa wote wa kisiasa

Wataalamu wa UM waitaka China kuheshimu haki za binadamu na kuwaachilia wafungwa wote wa kisiasa

Wataalamu wa Umoja wa mataifa wamejiunga na wale wanaounga mko uamuzi wa kamati ya kutoa tuzo la amani la Nobel baada ya kumtunuku Liu Xiaobo tuzo la amani la Nobel la mwaka 2010 na kutoa wito wa kuachiliwa kwake mara moja.

Liu Xiaobo alishiriki kwenye maandamano ya Tiananmen Squre mjini Beijing mwaka 1989 , akahudumu kama mhadhiri kwenye chuo kimoja mjini Beijing na pia kuchapisha makala yaliyotoa wito wa kuheshimiwa kwa haki za binadamu nchini humo. "Liu Xiaobo anatajwa kama mtu shubavu kwa kutetea haki za binadamu ambaye mara kwa mara alitaka kuheshimiwa kwa haki za binadamu nchini china. Wataalamu hao wa UM wanasema kuwa wamekaribisha kutambuliwa kwake. mwezi Disemba mwaka 2005 Xiaobo alihukumiwa kifungo cha miaka 11 gerezani hukumu ambayo wataalamu wa UM wanasema kuwa ni ukiukaji wa haki za za binadamu za kimataifa. Wanasema kuwa kulikuwa na utata kwenye kesi hiyo unayohusina na masuala ya kuendeshwa kwa njia isiyo ya haki.