Skip to main content

Mtuhumiwa wa uhalifu wa kivita nchini DRC atiwa mbaroni Ufaransa

Mtuhumiwa wa uhalifu wa kivita nchini DRC atiwa mbaroni Ufaransa

Mtuhumiwa wa uhalifu wa kivita na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemocracy ya Congo Callixte Mbarushimana ametiwa mbaroni nchini Ufaransa

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC hivi karibuni ilitoa warrant ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo anayedaiwa kutenda jinai hizo katika eneo la Kivu, nchini Congo.

Bwana Callixte  ambaye ni raia wa Rwanda anadaiwa kuongoza harakati kadhaa kwa kushirikiana na vikundi vya waasi na kuangamiza maisha ya raia katika maeneo la mbalimbali ya Kusin na Kaskazini mwa jimbo la Kivu.

Mamlaka za dola nchini Ufaransa zimesema kuwa zinaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo hadi hapo atapotakiwa kupanda kizimbani kujibu mashtaka dhidi yake