Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya mfanyakazi wake Afghanistan

UM walaani mauaji ya mfanyakazi wake Afghanistan

Umoja wa Mataifa umelaani vikali mauaji ya mfanyakazi wa kutoa misaada raia wa Uingereza aliyekuwa akihudumu nchini Afghanistan ambaye alitekwa nyara na baadaye kuarifiwa kuwa alikuwa ameuwawa.

Bi Linda Norgrove ambaye pia alikuwa akifanya kazi chini ya kivuli cha usamaria mwema alitekwa nyara mwezi uliopia katika Jimbo la Kunar lililoko eneo la Mashariki.

Akizungumzia kitendo hicho Naibu Mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya misaada ya kiutu huko Afghanistan Robert Watkins amesema kuwa kifo cha mtumishi huyo ni pigo kubwa kwa raia wa nchi hiyo kutokana na namna alivyojitoa kuwatumikia.

Amesema kushamiri kwa vitendo vya utomiaji mabavu na ghasia kwa wafanyakazi wanaotoa misaada ya kiutu katiika eneo hilo, vinapaswa kukomeshwa na kulaaniwa na kila mpenda amani.