Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Burundi warejea nyumbani baada ya miongo mitatu ugenini

Wakimbizi wa Burundi warejea nyumbani baada ya miongo mitatu ugenini

Mamia ya wakimbizi wa Burundi wamevuka mpaka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kurejea nyumbaniwiki hii.

Awamu ya kwanza ilikuwa na wakimbizi 240 na walisafirishwa kwa malori ya UNHCR wamesafirishwa jumanne ya wiki hii wakiwa ni miongoni mwa wakimbizi 10,000 wanaotarajiwa kurudi nyumbani Burundi katika miezi michache ijayo,

Kuna jumla ya wakimbizi 165,000 wa Burundi DRC na karibu 80,000 katika nchi jirani na Burundi. Kwa zaidi ya miezi sita iliyopita zaidi ya nusu wamerejea kwa hiyari , Burundi pia inahifadhi wakimbizi 41,000 wa Congo na mpango huu wa pande mbili wa kurejea kwa hiyari ni matokeo ya makubaliano kati ya UNHCR, Burundi na DRC.Mwandishi wetu Ramadhan Kibunga ameshuhudia wakimbizi hao wakiwasili nyumbani na kutuandalia makala hii.