Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yatoa msaada wa dharura Chad kukabili kipundupindu

UNICEF yatoa msaada wa dharura Chad kukabili kipundupindu

Shirika la Umoja wa Mataifa UNICEF limeanza kutoa msaada wa dhalura nchini Chad ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliosababishwa na mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo mwezi July mwaka huu.

Hali inaarifiwa kuwa mbaya zaidi katika eneo la mpaka wa Cameroon na mji mkuu wa N'Djamena,ambapo kwa wastani watu 50 wanaugua ugonjwa huo kwa siku. Hadi sasa tayari watu 112 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo .

Mwakilishi wa UNICEF nchini humo Dr Marzio Babille amesema mashirika mbalimbali ikiwemo WHO pamoja na Wizara ya Afya yameongeza juhudi ili kudhibiti ugonjwa huo