Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfungwa wa Uchina ashinda tuzo ya amani ya nobel 2010

Mfungwa wa Uchina ashinda tuzo ya amani ya nobel 2010

Mchina Liu Xiaobo ambaye kwa sasa yuko kifungoni ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya amani ya nobel kwa mwaka huu 2010.

Akitangaza ushindi huo mjini Oslo Norway, Rais wa kamati ya Nobel Thorbjoern Jagland amesema bwana Liu alikuwa msitari wa mbele na kuwa ishara ya kupigania haki za binadamu nchini Uchina. Hata hivyo duru za habari zimenukuliwa zikisema serikali ya Uchina imelaani tuzo hiyo na kusema itatia dosari uhusiano uliopo baina ya Uchina na Norway.

Kwa mujibu wa nmsemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Uchina Ma Zhaoxu, Liu Xiaobo ni mhalifu aliyekiuka sheria za Uchina, ni kukikuka misingi ya tuzo hiyo , ni kashifa kwa tuzo yenyewe na kwa kamati ya nobel kumpa tuzo mtu kama huyo.