Baada ya machafuko Kyrgystan sasa kuna matumaini:UNHCR

Baada ya machafuko Kyrgystan sasa kuna matumaini:UNHCR

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo amesema kuna hatua nzuri zilizopigwa kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa ndani na wanaorejea nyumbani miezi mine baada ya machafuko kuzuka Kusini mwa Kyrgystan.

Machafuko yaliyozuka mwezi Juni mwaka huu kwenye miji ya Osh na Jalalabad kati ya makabila ya Krgy na Uzubek, na kuathiri watu takriban laki tano, wengine laki nne kukimbia makazi yao na kwenye nchi jirani ya Uzbekistan. Wakati wa machafuko hayo pia nyumba 1700 zilichomwa na 2000 zaidi kuharibiwa. George Njogopa ana maelezo.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Maeneo kadhaa ya Kusini mwa nchi hiyo ikiwemo Osh na Jalalabad yalishuhudia machafuko makubwa yaliyozuka mwezi June, na kuathiri maisha ya maefu ya watu. Wengi kwenye machafuko hayo walipoteza nyumba zao zilizoharibiwa vibaya na wengine kulazimika kukimbilia ukimbizoni nje ya nchi.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR,likishirikiana na taasisi nyingine za kuwasaidia wakimbizi, limeanza kujenga makazi ya muda ili kuwasaidia waathirika hao pamoja na kutoa huduma za kiafya na mahitajio muhimu kwa binadamu.

Kyrgyzstan inatazamiwa kufanya uchaguzi wa Bunge mwishoni mwa juma hili,na UNHCR inaona kuwa hali hiyo itaharakisha kurejesha hali ya utulivu zaidi.