Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Iraq Syria wasita kurejea nyumbani

Wakimbizi wa Iraq Syria wasita kurejea nyumbani

Utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR uliofanyika hivi karibuni kuhusu wakimbizi wa Iraq wanaoishi Syria umebaini kwamba wengi wao bado wanasita kurejea nyumbani moja kwa moja.

Utafiti huo umefanyika mwezi Julai na Agosti mwaka huu, na familia 498 wakiwakilisha watu zaidi ya 2000 na wamesema kuna sababu nyingi zinachangia hali ya kuhofia kurejea nyumbani. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

Ameongeza kuwa utafiti kama huo pia umefanyika kwenye mpaka wa Iraq na Jordan na umebaini sababu kama hizo na watu wote 364 waliohojiwa hakuna hata mmoja mwenye mpango wa kurejea nyumbani.