Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Charles Petrie ajiuzulu kama mwakilishi wa UM Burundi

Charles Petrie ajiuzulu kama mwakilishi wa UM Burundi

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini amejiuzulu waadhifa huo.

Mwanadiplomasia huyo Mfaransa mwenye asili ya Uingereza amehudumu kwenye Umoja wa Mataifa kwa takribani miaka 20.

Aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Katibu Mkuu nchini Burundi mwezi Aprili mwaka jana akiwa na jukumu la kusimamia mchakato wa uchaguzi uliomalizika mwezi Agosti mwaka huu. Kutoka Bujumbura mwandishi wetu Ramadhani Kibuga ana maelezo zaidi

(RIPOTI YA RAMADHAN KIBUGA)