Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka ufadhili zaidi kuboresha chanjo kwa wote

Ban ataka ufadhili zaidi kuboresha chanjo kwa wote

Akisisitiza haja ya kuwekwa kwa usawa kwenye utoaji kinga na chanjo ili kunusuru afya za mamilioni ya watu ulimwenguni kote, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyatolewa mwito mataifa fadhili kuongeza ufadhili wake kwenye mfuko maalumu wa umoja huo ambao unashabaya ya kutoa kinga kwa wale wenye uhitajio mkubwa tena kwa muda muafaka.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000, mfuko huo unajulikana kama GAVI,yaani mpango wa Umoja wa Mataifa unaokusanya nguvu kwa ajili ya kutoa kinga na chanjo, umeweza kuwafadia watoto milioni 257 waliopatiwa huduma za kinga.

Shabaya kubwa ya mpango huo ni kuona kwamba kunapatikana na chanjo na kinga za kutosha ili kuzuia vifo vya mamilioni ya watu duniani kote,ili hatimaye kufikia moja ya malengo ya maendeleo ya mellenia.

Akizungumza kwenye hafla iliyoandaliwa na mfuko huo, Ban pamoja na kupongeza juhudi hizo zilizofikiwa sasa, lakini ametaka kuongezwa kwa mafungo ya fedha ili matunda yake yaweze kuwafikia watu wengi zaidi.