Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA yapendekeza mabadiliko kwa kinu cha nyuklia Ufaransa

IAEA yapendekeza mabadiliko kwa kinu cha nyuklia Ufaransa

Kundi la wataalamu wa kimataifa likiongozwa na shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA limependekeza kinu cha kinyuklia cha Ufaransa kufanyiwa marekebisho ya kiusalama baada ya kuzuru kinu hicho kilicho mashariki mwa Ufaransa.

Wataalamu hao kutoka nchi tisa walikikagua kinu hicho cha Saint-Alban kwa mwaliko wa serikali ya Ufaransa ambapo waliangazia masuala ya usimamizi , mafunzo , usalama wa miale na mengineyo. Wataalamu hao pia walipendekeza watu walioruhisiwa kuingia kwenye chumba kinachodhibiti kinu hicho.

Nao wasimamizi wa kinu hicho waliwahakikishia wataalamu hao kuwa watashughulikia sehemu zinazohitaji marekebisho na kuliomba shirika la IAEA kukitembelea tena kinu hicho baada ya miezi 18. Hii ni mara ya 158 kundi la wataalumu wa usalama wa vinu vya kinyulia kuendesha shughuli kama hiyo inayofahamika kama OSART tangu ianzishwe mwaka 1982.