Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajumbe wa baraza la usalama wazuru kituo cha UM Uganda

Wajumbe wa baraza la usalama wazuru kituo cha UM Uganda

Ujumbe kutoka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ulitembelea kituo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na ugavi na usafirishaji wa vitu kwenye mji wa Entebbe nchini Uganda ambapo walijulishwa kuhusu shughuli za kituo hicho na pia kukutana na rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kuelekea nchini Sudan.

Wakiwa mji wa Sudan kusini Juba, wajumbe hao watakutama na viongozi wa neo hilo na kuelezwa kuhusu huduma za UM nchini Sudan.

Wajumbe hao wanaitembelea Sudan wakati wenyeji wa eneo la kusini mwa nchi wanapojiandaa kupiga kura tarehe 9 mwezi Januari mwaka ujao ya kuamua ikiwa wangetaka kujitenga na eneo la kaskazini huku wenyeji wa eneo la Abyei lililo kati kati mwa Sudan nao wakipiga kura ya kuamua iwapo watajiunga na kusini au kaskazini.

Kura hiyo ya maoni itakuwa awamu ya mwisho ya kutekelezwa kwa makubalino ya mwaka 2005 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo miwili kati ya serikali ya kaskazini na wanajeshi wa kundi la Sudan peoples's Liberation Movement SPLM lililo kusini.