Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM wa masuala ya utesaji kuzuru Ugiriki

Mwakilishi wa UM wa masuala ya utesaji kuzuru Ugiriki

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya utesaji anatarajiwa kuzuru Ugiriki kuangazia masuala ya haki za binadamu.

Manfred Nowak ataanza ziara hiyo Oktoba 10 hadi Oktoba 20, na itakuwa ni ziara ya kwanza ya mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa nchini humo kukusanya taarifa za ukiukaji wa haki za binadamu, utesaji, ukatili miwngine, udhalilishaji na adhabu. George Njogopa anayo taarifa.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na mtaaalamu aliyeidhinishwa na Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa nchini humo kufutilia vitendo vinavyoambatana na utesaji, ukatiri na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Bwana Nowak ambaye ziara yake hiyo imepata baraka za serikali nchini humo amesema kuwa anaamini kazi atayoifanya inawakilisha utashi sahihi wa kutaka kutathmini hali jumla ya mambo na pia kutaka kuamsha mwamko mpya kwa serikali namna inavyoweza kujijenga upya kuhusiana na uimarishwaji wa haki za binadamu.

Akiwa nchini humo mtaalamu huyo atakutana na makundi mbalimbali ikiwemo maafisa wa serikali, mashirika ya kiraia na mashirika ya kimataifa pamoja na wawakilishi wake.