Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Burundi ajiuzulu

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Burundi ajiuzulu

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi amejiuzulu wadhifa huo wiki hii.

Balozi Charles Petrie amejiondoka pia kwenye shughuli zote za Umoja wa Mataifa nchini humo akisema ni kutokana na sababu binafsi. Mwanadiplomasia huyo Mfaransa mwenye asili ya uingereza amehudumu kwenye Umoja wa Mataifa kwa takribani miaka 20.

Aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Katibu mkuu nchini Burundi mwezi Aprili mwaka jana akiwa na jukumu la kusimamia mchakato wa uchaguzi uliomalizika mwezi Agosti mwaka huu. Kutoka Bujumbura mwandishi wetu Ramadhani Kibuga ana maelezo zaidi

(RIPOTI YA RAMADHAN KIBUGA)