Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa baraza la usalama unaendelea na ziara Sudan

Ujumbe wa baraza la usalama unaendelea na ziara Sudan

Ujumbe wa baraza la usalama unaozuru Afrika hii leo umetembelea eneo la El-Fasher kwenye jimbo la Darfur.

Kwa mujibu wa vikosi vya pamoja vya kulinda amani kweny jimbo hilo ambavyo ni vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa afrika UNAMID ujumbe huo zuru Sudan mahsusi kwa ajili ya kutathimini maandalizi ya kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika Januari mwakani. Pia ujumbe huo umekutana na wawakilishi wa UNAMID, viongozi wa Darfur na timu ya Umoja wa Mataifa iliyoko Darfur.

Kabla ya kuwasili Juba jana ujumbe huo ulikuwa nchini Uganda ambako ulikutana na Rais Yoweri Museveni aliyetoa wito wa msaada wa kimataifa ili kuzisaidia nchi za Afrika kuongeza vikosi vya kulindamani nchini Somalia AMISOM. Museveni ametoa ahadi ya kuongeza vikosi vyake ili kulifanya jeshi la AMISOM kufikisha wanajeshi 20,000.

Hivi sasa jeshi hilo lina wanajeshi 7200 na wanajeshi 4000 kati hao wanatoka Uganda. Amesema Umoja wa Mataifa, nchi tajiri za magharibi na nchi tajiri za Afrika wana jukumu la kusaidia ili kumaliza uasi na ugaidi nchini Somalia.